IQNA

Nakala ya kwanza ya maandishi ya mkono ya Qur'ani inahifadhiwa Yemen

15:46 - August 07, 2011
Habari ID: 2166666
Nakala ya kwanza ya maandishi ya mkono ya Qur'ani Tukufu ambayo iliandikwa miaka 70 baada ya kufariki dunia Mtume Muhammad SAW inahifadhiwa katika Msikiti wa Jamia wa Sanaa nchini Yemen.
Gazeti la al Youm al Sabi la Misri limeripoti kuwa nakala ya kwanza ya Qur'ani iliyoandikwa kwa mkono ambayo iligunduliwa katika msikiti wa kwanza kabisa kujengwa nchini Yemen mjini Sanaa iligunduliwa mwaka 1972 na nakala hiyo nadra na yenye thamani kubwa inahifadhiwa katika Msikiti wa Jamia.
Nakala hiyo ya Qur'ani ni ya kipindi cha karne ya saba au nane Miladia na wataalamu wa nakala za maandishi ya mkono wanaamini kwamba iliandikwa miaka 70 baada ya kufariki dunia Mume Mumammad SAW.
Mwaka 1972 ziligunduliwa nakala za maandishi ya mkono katika Msikiti wa Jamia wa Sanaa ambazo baadhi yao hazikuwa Qur'ani. Nakala hizo zligunduliwa na wajenzi waliokuwa wakikarabati msikiti huo ambao ndio mkongwe zaidi nchini Yemen. Msikiti huo ulijengwa mwaka wa 6 baada ya hijra ya Mtume SAW kutoka Makka na kwenda Madina.
Jambo la kuvutia zaidi ni kuwa wataalamu wa masuala ya Mashaiki wa Ulaya ambao walikuwa wakidai kuwa Qur'ani imefanyiwa mabadiliko walibakia bumbuazi baada ya kuona nakala hiyo ambayo imethibitisha kwamba kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu hakijafanyiwa mabadiliko ya aina yoyote katika kipindi chote cha historia. 838588
captcha