Kikao hicho kinatazamiwa kuanza saa tatu na nusu hadi saa tano usiku,
Kikao hicho kitajumuisha hotuba ya Hujjatul Islam Dashti na katibu wa kikao Hujjatul Islam Sayyed Ali Sadat Fakhr.
Hiki kitakuwa kikao cha nne katika mfululizo wa vikao vilivyoandaliwa na kitengo cha utafiti katika maonyesho hayo.
Vikao vya kwanza vitatu vilihusu, ‘Qur’ani na Utamaduni wa Wakati’, ‘Msingi wa Kufahamu Hadithi za Tafsiri Katika Al Mizan’ na ‘Nafasi ya Hadithi katika Tafsiri ya Qur’ani’.
Kitengo cha utafiti katika maonyesho ya Qur’ani ya Tehran pia kimeandaa warsha mbalimbali kuhusu Qur’ani Tukufu. 838943