IQNA

Mashindano ya Qur’ani ya Dubai yaanza

14:14 - August 08, 2011
Habari ID: 2167163
Mashindano ya 15 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Dubai yameanza katika Kituo cha Utamaduni na Sayansi katika eneo la Al Mamzar Dubai huko Umoja wa Falme za Kiarabu.
Ahmad al Zahid Mkuu wa Kitengo cha Habari katika mashindano hayo amesema mashindano hayo yana washiriki kutoka zaidi ya nchi na jamii 160 duniani.
Ameongeza kuwa idadi ya washiriki mwaka huu ni zaidi ya mwaka jana. Zahid amesema kuwa, ‘Mahafidhi watafanyiwa mtihani wa awali kuainisha viwango vyao’.
Mashindano hayo ya siku 12 yatamalizika Agosti 18 na kwa mara ya kwanza mshiriki mwenye umri mdogo zaidi, mvulana mwenye umri wa miaka minane kutoka Ireland, anashiriki.
Kundi la kwanza la mahufadhi ni Abdul Wahid Masomi (Afghanistan), Hissein Youssouf (Jamhuri ya Afrika ya Kati), Aras Ass’ad Ibrahim Bany Shamsah (Jordan), Alhassan Ezudeen (Ghana), Iskandarov Nasrullo (Kyrgyzstan), Algassimou Bah (Guinea) and Nuradinov Shamil (Russia).
839251
captcha