Vijana Waislamu na wasiokuwa Waislamu nchini Bolivia wamehusika katika uchapishaji wa jarida hilo ambalo limezinduliwa kwa munasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Toleo la kwanza la jarida hilo lina maudhui kama vile ‘Simon Bolivar na Qur’ani’, ‘Siku ya Uhuru Bolivia’, ‘Kufahamu Mwezi wa Ramadhani’, ‘Waislamu wa Bolivia Mwezi wa Ramadhani’, ‘Uhuru wa Wanawake kwa Mtazamo wa Uislamu’ na ‘Ugaidi kwa Mtazamo wa Uislamu’.
Mhariri Mkuu wa Jarida hilo ni mwanamke wa Kishia ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Bolivia. Amesema toleo la pili litachapishwa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo huadhimishwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
838177