IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Misri kuanza 19 Ramadhani

14:17 - August 08, 2011
Habari ID: 2167187
Mashindano ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Misri yanatazamiwa kuanza tarehe 19 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Waziri wa Waqfu nchini Msiri Mohammad Abdul Faisal al Qusi amesema wizara yake imejitayarisha kikamilifu kuandaa mashindano hayo.
Washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani watashindana katika vitengo vitano na washindi watatunukiwa zawadi baada ya mashindano hayo. Wizara ya Waqfu ya Misri imesema nchi zaidi ya 80 zimealikwa kushiriki katika mashindano hayo yatakayomalizika tarehe 26 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mashindano hayo yatakuwa katika vitengo vya kuhifadhi Qur’ani kamili, tajweed, tafsiri ya juzuu moja ya Qur’ani, kuhifadhi juzuu 20 na tajweed, kuhifadhi juzuu 10 na tajweed na kuhifadhi juzuu tano na tajweed.
Mashindano ya mwaka huu pia yana kitengo maalumu cha nchi za wasio zungumza lugha ya Kiarabu ambao watashindano kuhifadhi juzuu sita za Qur’ani Tukufu.
839385
captcha