IQNA

Ahmad Nuina' ashiriki katika vikao vya kufarijika na Qur'ani Karbala

19:48 - August 08, 2011
Habari ID: 2167409
Vikao vya kufarijika na Qur'ani ambavyo tokea mwanzoni mwa mwezi huu wa Ramadhani vimekuwa vikifanyika katika Haram mbili za Imam Hussein na Hadhrat Abbas (as) huko katika mji mtakatifu wa Karbala viliendelea hapo jana Jumapili ambapo Ahmad Nuina, msomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Misri alishiriki.
Vikao hivyo ambavyo vinalenga kuhitimisha usomaji wa Qur'ani nzima katika mwezi huu mtukufu vimeandaliwa na idara ya haram zilizotajwa.
Wasomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Iraq na Misri wanashiriki katika vikao hivyo ambavyo vinahudhuriwa na wapenzi wa Qur'ani kutoka pande zote za Iraq na wageni wanaozuru makaburi ya Imam Hussein na Hadhrat Abbas (as).
Watu wanaoshiriki katika vikao hivyo wanasema kuwa vinatoa mfano bora wa kushirikiana wasomaji mashuhuri wa Qur'ani kutoka madhehebu mbili muhimu za Kiislamu za Suni na Shia katika kuimarisha umoja wa umma wa Kiislamu. 839301
captcha