Kwa mujibu wa Taasisi ya Kiutamaduni ya Tarjumi ya Wahyi, tarjumi nyingi za Qur'ani zilizoandikwa kwa mkono zimetimia kwa lugha za Kifarsi, Kituruki na Kiurdu lakini kwamba tarjumi nyingi kama hizo zilizoandikwa kwa lugha ya Kifarsi hazijachapishwa na hivyo kutowanufaisha watu wengi.
Imesema miongoni mwa tarjumi kama hizo chache zilizochapishwa ni pamoja na tafsiri ya Tabari iliyoandikwa katika karne ya nne Hijiria.
Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi hiyo akiba yenye thamani kubwa ya tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya kifarsi ina maneno muhimu ya kale na ya asili ambayo yana maana ya kina kuhusiana na taaluma mbalimbali zinazomuhusu mwanadamu.
Taasisi hiyo inaonyesha vitabu na tarjumi kadhaa mpya za Qur'ani zilizotarjumiwa kwa lugha tofauti katika maonyesho ya 19 ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran. 837306