IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa viziwi yaanza Kuwait

19:42 - August 08, 2011
Habari ID: 2167411
Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya viziwi yameanza leo Jumatatu nchini Kuwait na yataendelea hadi Jumatano Agosti 10.
Mashindano hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa shirika la huduma za simu za mkononi la Zein, Tasisi ya Wakfu kwa ajili ya Vizazi vya Qur'ani na Shirika la Utamaduni na Masuala ya Kijamii la Raya. Akizungumzia suala hilo Abdallah al-Jad'an Mkurugenzi mwandamizi wa shirika la Zein amesema kuwa hayo ni mashindano ya kwanza ya aina yake kuwahi kufanyika katika eneo la Ghuba ya Uajemi. Amesema mashindano mengine makubwa kama hayo yamepangwa kufanyika mwakani ambapo nchi 11 za Kiislamu zitashirikishwa. Amesema shirika lake limepata fahari ya kuandaa mashindano hayo kwa ajili ya tabaka hili muhimu katika jamii na kwamba yamefanyika kwa shabaha ya kuwahamasisha wajishughulishe zaidi na usomaji na hifdhi ya Qur'ani Tukufu pamoja na kutekeleza mafundisho ya kitabu hicho kitakatifu. 839229
captcha