Shirika rasmi la habari la Imarati WAM limeripoti kuwa mashindano hayo yanafanyika kwa kaulimbiu ya “Warattilil Qur’ana Tartila” yakiwashirikisha vijana na mabarobaro wenye umri wa kati ya miaka 12 na 18.
Mashindano hayo yanasimamiwa na Baraza Kuu la Masuala ya Familia la Sharja ikiwa ni katika shughuli za tamasha ya Ramadhani makhsusi kwa ajili ya vijana.
Washiriki wanachuana kusoma juzuu ya mwisho ya Qur’ani Tukufu na sura ya Qaf.
Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha vijana wa Sharja Said batti Hadid anasema mashindano hayo yanafanyika kwa shabaha ya kugundua vipawa vya vijana katika masuala ya Qur’ani, kukuza uwezo wao na kuwafunza sharia za kiraa na tajwidi. Ameongeza kuwa lengo jingine ni kuimarisha thamani za kidini na kuwafanya vijana washikamane na kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu. 840002