IQNA

Benki ya Maendeleo ya Kiislamu yadhamini ukarabati wa madrasa za Qur'ni nchini Senegal

17:11 - August 09, 2011
Habari ID: 2167972
Benki ya Maendeleo ya Kiislamu BID jana Jumatatu ilichukua uamuzi wa kutenga franka bilioni 9 kwa ajili ya kukarabati shule na madarsa za Qur'ani nchini Senegal.
Katika mazungumzo yaliyofanyika hivi karibuni kati ya Bubakr Sidi Ba Naibu Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kiislamu na Karim Wade, Waziri wa Nishati na Uchukuzi wa Senegal, benki hiyo imekubali kudhamini ukarabati, ustawishwaji na ujenzi wa shule hizo nchini humo.
Kwa mujibu wa mapatano hayo, baada ya kupokea fedha hizo, serikali ya Senegal itaanzisha madrasa mapya 416 katika shule 64 za Qur'ani na kuajiri walimu wapya wapatao 224 kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Qur'ani katika madrasa hizo.
Waziri aliyetajwa wa Senegal amesema mwishoni mwa mazungumzo hayo kwamba fedha hizo zitapewa Wizara ya Elimu ili iandae uwanja wa ukarabati na ujenzi wa shule hizo za Qur'ani kote nchini. 839932
captcha