Mashindano hayo yanayofanyika chini ya nara ya 'Wa Rattil al-Qur'ana Tartilla' yanawashirikisha vijana wadogo walio na umri wa kati ya miaka 12 hadi 18. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Idara Kuu ya Vituo vya Vijana na ambayo inafungamana na Halmashauri Kuu ya Masuala ya Familia ya Sharjah yanafanyika katika kalibu ya shughuli za tamasha la Ramadhani maalumu kwa vijana.
Washiriki wanachuana kuhifadhi juzuu ya 30 ya Qur'ani Tukufu na kusoma Surat Qaf. Waandaaji wa mashindano hayo wanasema kuwa yameandaliwa kwa madhumuni ya kudhihirisha vipawa na vipaji vya washiriki kutoka Sharjah katika usomaji na hifdhi ya Qur'ani Tukufu, ili kuvikuza vipawa hivyo na hatimaye kuimarisha ufahamu wao kuhusiana na mafundisho ya kitabu hicho cha mbinguni.
Wanasema washindi 16 wa hatua ya mwanzo ya mashindano hayo watachaguliwa ili kushiriki katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo. Mashindano hayo ya Sharjah yamepangwa kukamilika hapo leo Jumatano. 840002