IQNA

Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya Qur’ani Tehran kufunguliwa

13:21 - August 10, 2011
Habari ID: 2168363
Kitengo cha Kimataifa katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani Tehran kinafunguliwa Jumatano ya leo katika hafla itakayohudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran na vilevile mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu.
Hafla hiyo itahudhuriwa pia na wasanii na watarjumi wa Qur’ani kutoka Bangladesh, Pakistan, Afghanistan, Tunisia, Ufilipino, Indonesia, Bosnia, Sudan, Uturuki, Syria, Azerbaijan, Kuwait, Uchina, Lebanon, Kenya na India.
Katika kitengo hicho cha kimataifa, kunafanyika juhudi za kubadilishana mawazo na fikra kati ya wasomi na wataalamu wa Qur’ani kutoka maeneo mbalimbali duniani.
840550
captcha