IQNA

Nakala ya Qur'ani inayonasibishwa kwa Imam Ali AS kuzinduliwa

16:17 - August 10, 2011
Habari ID: 2168644
Mkurugenzi wa kitengo cha kimataifa cha Mashindano ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran amesema kuwa msahafu unaonasibishwa kwa Imam Ali bin Abi Twalib AS ambao metarjumiwa nchini Pakistan, utazinduliwa katika maonyesho hayo.
Ali Ridha Ismaili amesema kongamano la Qur'ani, Kitabu cha Mwamko pia litafanyika katika maonyesho hayo yanayoendelea mjini Tehran ambapo wageni waalikwa kutoka nchi za nje watawasilisha makala zao.
Amesema kuwa kongamano hilo litafanyika tarehe 14 Agosti na kuhudhuriwa na maulamaa wa Kiislamu. Amesisitiza kuwa moja na ratiba za kongamano hilo ni kuzindua msahafu ambao umeandikwa kwa hati za Amirul Muuminin Ali bin Abi Twalib AS. 840747


captcha