IQNA

Mashindano ya Qur'ani kufanyika jimboni Hawaii, Marekani

17:14 - August 10, 2011
Habari ID: 2168658
Mashindano ya hifdhi na tafsiri ya Qur'ani Tukufu yamepangwa na Umoja wa Waislamu wa Jimbo la Hawaii nchini Marekani kufanyika hapo tarehe 26 Agosti katika makao makuu ya umoja huo.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo, yamepangwa kufanyika katika makundi matatu ya hifdhi na tafsiri ya sura 30, 20 na 10 za mwisho za Qur'ani Tukufu. Mashindano hayo yatafanyika bila kuzingatia umri wa washiriki na washindi kutangazwa baadaye alasiri siku hiyohiyo ya mashindano.
Muungano huo wa Waislamu pia unatekeleza ratiba maalumu za hotuba katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ambapo wanazuoni wa jimbo hilo wanazungumzia masuala mbalimbali yanayohusiana na ulimwengu wa Kiislamu. 840673
captcha