Kitengo cha kimataifa cha Maonyesho ya 19 ya Qur’ani Tehran kimefunguliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa serikali, wasomi, na wageni waalikwa kutoka nje ya nchi.
Shirika la habari la IQNA limeripoti kuwa kitengo cha kimataifa cha Maonyesho ya 19 ya Qur’ani Tukufu ya Tehran kina sehemu tatu kuu ambazo ni utafiti wa masuala ya Qur’ani, kitengo cha tarjumi na sehemu ya wachapishaji, wanaharakati wa masuala ya Qur’ani Tukufu na wasanii.
Katika kipindi chote cha maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani mjini Tehran, wageni 40 kutoka nchi za nje watakutana na kufanya mazungumzo na vituo na shakhsia wa masuala ya Qur’ani na utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Baadhi ya wageni hao wanawakilishi nchi za Ujerumani, Bangladesh, India, China, Kuwait na Kenya.
Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani yalianza hapa jijini Tehran tarehe 29 Julai na yataendelea hadi tarehe 26 Agosti. 841175