IQNA

Taswira ya "Majina ya Allah" katika maonyesho ya Qur'ani Tehran

17:28 - August 13, 2011
Habari ID: 2169860
Taswira ya majina 99 ya Allah yaliyoandikwa na Gori Yusuf Hussein yanaonyeshwa katika kibanda cha India katika Maonyesho ya 19 ya Qur'ani mjini Tehran.
Ubao wa inchi 36x54 ni moja kati ya kazi zilizowasilishwa na msanii huo kutoka India katika kitengo cha kimataifa cha maonyesho ya Qur'ani ya Tehran yaliyofunguliwa Agosti 10.
Kazi hii bora ya kisanii ya Qur'ani imeandikwa kwenye ngozi na karatasi kwa kutumia wino na mimea.
Mtaalamu huyo wa sanaa za Kiislamu pia ameandika Bismillah pamoja na sura kadhaa kama vile Baqarah, Yasin na Fatiha.
Jina la Ka'aba, majina ya Allah, Mtume SAW na Ahlul Bayt AS ni kati ya kazi zilizowasilishwa katika maonyesho hayo.
841755
captcha