al Suwaidi amesema kuwa kamati ya tathmini ya Mashindano ya 15 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai imeamua kuwaondoa washiriki hao 11 katika mashindano hayo kutokana na udhaifu na kiwango chao cha chini.
Amesema kuwa mwakilishi wa Kosovo katika mashindano hayo pia amejiondoa na kwa msingi huo ni washiriki 78 kutoka nchi 90 tu ndio wataochuana katika kinyang'anyiro hicho.
Amesema mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani yanawashirikisha mahafidhi hodari na bora na kwamba sherehe za mwisho za mashindano hayo zitafanyika tarehe 20 Ramadhani. 842260