IQNA

Rais Ahmadinejad awatunuku nishani wanaharakati wa Qur'ani nchini Iran

14:15 - August 14, 2011
Habari ID: 2170079
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatunuku nishani ya juu kabisa maustadhi na maqarii 14 wa kimataifa.
Katika hafla ya Jumuiya ya Wanaharakati wa Qur'ani iliyofanyika Jumamosi usiku katika Ofisi ya Rais mjini Tehran Rais Ahmadinejad amesema kuwatunuku nishani wanaharakati hao wa Qur'ani ndio mwanzo.
Katika sherehe hiyo iliyodhudhuriwa pia na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Sayyid Muhammad Husseini, Rais Ahmadinejad ameelezea matumani kuwa wanaharakati wote wanaohudumia Qur'ani Tukufu nchini Iran wataenziwa. Rais wa Iran amesema Qur'ani Tukufu ni kitabu cha kumsimamia mwanadamu na jamii ya wanadamu.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Utamaduni Sayyeid Husseini ameelezea matumaini yake kuwa mwakani harakati hiyo ya kuwaenzi wanaohudumia Qur'ani itaendelea kwa njia bora zaidi.
Baada ya hafla hiyo washiriki walisali sala ya Magharibi na Ishaa na baada ya hapo walifuturu pamoja.
842488
captcha