IQNA

Nuskha 20,000 za Qur'ani zisizo na kibali zakusanywa Misri

14:21 - August 14, 2011
Habari ID: 2170215
Nuskha za Qur'ani zipatazo 20,000 ambazo zimechapishwa na kusambazwa bila kupata idhini ya Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya al-Azhar nchini Misr zimenaswa na kukusanywa na Idara Kuu ya Utafiti na Ulindaji wa Haki za Umiliki wa Kimaanawi ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Al-Yaum as-Sabi', Shirika la Uchapishaji la ad-Dhahir lilikuwa na lengo la kuchapisha Qur'ani hizo na kisha kuzisambaza sokoni katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Kufuatia hatua zilizochukuliwa na maafisa wa usalama, shirika hilo limefungwa na mmiliki wake kutiwa mbaroni ili kujibu mashtaka yanayohusiana na uchapishaji wa nuskha hizo bila kubali kutoka kwa idara husika.
Kufikia sasa idara iliyotajwa ya kutetea haki za umiliki wa kimaanawi imefanya kazi kubwa katika kufuatilia na kusaidia kutiwa mbaroni kwa wahalifu wanaokiuka sheria za uchapishaji na usambazaji wa vitabu nchini Misri. 842146
captcha