IQNA

Mashindano ya Qur'ani Morocco yaanza

14:25 - August 14, 2011
Habari ID: 2170293
Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu Morocco yajulikanayo kama "Zawadi ya Mfalme Mohammad wa Sita" yameanza Agosti 13 katika Msikiti wa al Sunnat katika mji wa Rabat.
Mashindano hayo yanadhaminiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Morocco na yatakuwa nawashiriki 221 wa kiume na 33 wa kike katika vitengo vya hifdhi na kiraa.
Waliofuzu katika mashindano ya kimikoa na kieneo ndio waliofika katika mashindano hayo ya kitaifa.
Hassan Jait Mkuu wa kitengo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika Wizara ya Wakfu ya Morocco amesema mashindano hayo yataendelea hadi tarehe 16 Agosti na kwamba jopo la majaji 10 ni kutoka Morocco. Ameongeza kuwa washindi watatunukiwa zawadi katika sherehe zitakazofanyika tarehe 17 Agosti. 842669
captcha