Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kiislamu wa Misri Abdulfadhil Alfusi amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa katika vitengo vya kuhifadhi Qur’ani kamili, tajweed, tafsiri ya juzuu moja ya Qur’ani, kuhifadhi juzuu 20 na tajuwidi, kuhifadhi juzuu 10 na tajuwidi na kuhifadhi juzuu tano na tajuwidi.
Ameongeza kuwa mashindano ya mwaka huu pia yana kitengo maalumu cha nchi za wasio zungumza lugha ya Kiarabu ambao watashindana kuhifadhi juzuu sita za Qur’ani Tukufu.
Majaji watakaosimamia mashindano hayo ni kutoka Misri, Saudi Arabia, Bahrain, Senegal, Syria, Algeria na Oman.
841964