Mtoto Fadhl Azeem amefanikiwa kupata nafasi ya kwanza katika mashindano hayo yaliyowashirikisha mamia ya mahafidhi kutoka nchi 35 duniani.
Katika mashindnao hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mjini Makka, washiriki walifanyiwa mtihani wa lahani, kiraa na jinsi ya kusoma aya za Qur'ani Tukufu.
Msimamizi wa mashindano hayo karii Muhammad Yusuf amesema hii ni mara ya kwanza kwa mtoto kutoka Pakistan kushinda mashindano hayo kwani kila mwaka mamia ya mahafidhi wanaoshiriki katika mashindano hayo huwa wazungumzaji wa lugha ya Kiarabu, tofauti na mtoto huyo wa Pakistan.
Ameongeza kuwa Fadhl amewashinda makarii wenzake kutoka Misri na Uturuki ambao ni mashuhuri kwa usomaji wao sahihi wa aya za Qur'ani. 842353