Kwa mujibu wa tovuti ya al Bawaba, mpango huo unadhaminiwa na Idara ya Forodha Dubai kwa lengo kwa kuwapa watoto wa wafanyakazi wa idara hiyo na jamii nzima ya Dubai fursa ya kuhifadhi Qur’ani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Faryal Tawakkul Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Jamii katika Idara ya Forodha ya Dubai amesema mpango huo unafanyika chini ya nara ya ‘Warattilil Qur'ana Tartila’. Malengo mengine ya mpango huo ni kustawisha utamaduni wa Kiislamu na kuongeza kiwango cha umaanawi miongoni mwa watoto, amesema. Tawakkul ameongeza kuwa mpango huo pia unalenga kuwahimiza watoto watumie vizuri wakati wao wa mapumziko.
842946