Akizungumzia suala hilo bungeni, Usama an-Nujaifi, Spika wa Bunge hilo ameitaka kamisheni inayoshughulikia masuala ya vyombo vya habari na mawasiliano ya bunge hilo kutoa tangazo la kupiga marufuku filamu hiyo inayopotosha ukweli wa kihistoria kwenye televisheni za Iraq.
Kikao hicho cha bunge kilifanyika kutokana na ombi la baadhi ya wabunge, Jumuiya ya Wanazuoni wa Kishia na Kisuni pamoja na mamarja' wa Iraq kwa lengo la kuzuia filamu hiyo isije ikawasha moto wa fitina za kimadhehebu nchini humo. 842877