IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur'ani kwa viziwi nchini Kuwait Waarifishwa

15:18 - August 15, 2011
Habari ID: 2170864
Washindi wa mashindano ya kimataifa ya hifdhi ya Qur'ani maalumu kwa viziwi ambayo yalifanyika nchini Kuwait tokea tarehe 8 hadi 10 za mwezi huu mtukufu wa Ramadhani wamearifishwa na kutunukiwa zawadi.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Wasat linalochapishwa Bahrain, mashindano hayo ambayo ni ya aina yake kuwahi kufanyika katika eneo la Ghuba ya Uajemi, yamezishirikisha nchi kadhaa za Mashariki ya Kati. Wawakilishi wa nchi za Kuwait, Morocco, Misri, Saudi Arabia, Oman na Bahraini walishinda nafasi za mwanzo katika makundi mbalimbali ya mashindano hayo.
Mashindano hayo ya viziwi ambayo ni ya pili kufanyika yamedhaminiwa na shirika la kimataifa la simu za mkononi la Zein la nchini Kuwait kwa ushirikiano wa Taasisi ya Wakfu kwa ajili ya Vizazi vya Qur'ani na vilevile Shirika la Utamaduni na Masuala ya Kijamii la Raya la nchini humo . 843088
captcha