IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur’ani Oman wazawadiwa

15:10 - August 15, 2011
Habari ID: 2171264
Washindi wa Mashindano ya 21 ya Qur’ani ya Sultan Qaboos nchini Oman watatunukiwa zawadi katika Msikiti wa Sultan Qaboos mjini Muscat Jumatatu 15 Agosti.
Mshauri wa Sultan, Sheikh Abdullahi bin Ali al Qatabi atahudhuria hafla hiyo.
Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Sultan Qaboos katika vitengo vitano vya hifdhi na qiraa.
Watakaotunukiwa zawadi ni washindi 15 wakiwemo washiriki wenye ulemavu.
Pembizoni mwa hafla hiyo familia za washiriki zitaenziwa pamoja na zawadi maalumu kwa walio na umri wa chini.
Mashindano ya mwaka huu yalikuwa na washiriki 617 katika maeneo 17 ya Oman.
843416
captcha