IQNA

Shule ya kwanza ya watoto ya Qur'ani nchini Iraq kuanzishwa mjini Karbala

17:12 - August 16, 2011
Habari ID: 2171702
Shule ya kwanza ya watoto inayotoa mafundisho ya Qur'ani Tukufu inayoitwa Imam Hussein (as) imepangwa kufunguliwa hivi karibuni katika mji mtakatifu wa Karbala.
Shule hiyo imejengwa kwa udhamini wa Taasisi ya Dar al-Qur'an al-Karim inayofungamana na Idara ya Haram ya Imam Hussein (as) mjini humo.
Wasimamizi wa shule hiyo wanasema kuwa inaanzishwa kwa madhumuni ya kueneza utamaduni na mafundisho ya Qur'ani Tukufu nchini Iraq na kuwazingatia zaidi kidini watoto walio na umri mdogo wa nchi hiyo. Wanasema lengo ni kulea na kuwafundisha wanafunzi walio na umri mdogo mafundisho na utamaduni wenye thamani kubwa wa Qur'ani Tukufu.
Mbinu za kisasa za mafunzo na zinazowavutia watoto zitatumika katika kufikia lengo hilo.
Wakuu wa shule hiyo pia wanasema kuwa wataalamu na walimu walio na ujuzi na uzoefu mkubwa wa kufunza watatumika katika kutoa mafunzo ya Qur'ani katika shule hiyo ambayo ni ya kwanza ya aina yake nchini Iraq. 843890
captcha