IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur’ani Tanzania watangazwa

11:45 - August 17, 2011
Habari ID: 2172221
Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani yamefanyika katika Shule ya Sekondari Al-Haramain katika mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam na washindi kukabidhiwa zawadi Agosti 14.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameshiriki katika sherehe za kutoa zawadi kwa washindi.
Mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya Qur'ani ya kuhifadhi juzuu 30 alikuwa Mariam Salum Mohamed mwenye umri wa miaka 15 kutoka Madrassa Tarbiyatul-Islamiyah ya Kisiwa cha Pemba, wa pili alikuwa Aisha Faki Khatib mwenye umri wa miaka 18, kutoka, Madrasa Istiqama ya Kisiwa cha Pemba. Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Shaame Said Shaame mwenye umri wa miaka 18 kutoka, Madrasa ya Ibun Jazary katika eneo la Vikindu mjini Dar-es-Salaam.
Kati ya waliodhudhuria sherehe za kutoa zawadi kwa washindi ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake, Baraza Kuu la Waislam Tanzania Bi, Shamim Khan.
844671
captcha