IQNA

Kazi za Kaligrafia ya Qur’ani Iran zaonyeshwa Qatar

11:53 - August 17, 2011
Habari ID: 2172234
Maonyesho ya Kaligrafia ya Qur’ani iliyotayarishwa na mtaalamu Muirani Abbas Rahmani yamefunguliwa Agosti 16 katika Taasisi ya Utamaduni ya Al Hayy nchini Qatar.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Sharq, maonyesho hayo yamefunguliwa na Hamd bin Abdul Azizi al Kuwari Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Turathi wa Qatar.
Seyyid Ali Imamzadeh, mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran mjini Qatar amesema maonyesho hayo yataendelea hadi Agosti 25.
Maonyesho hayo yanajumuisha hati za Nastaliq ambazo hutumika katika kaligrafia ya Iran.
Ameelezea matumaini kuwa maonyesho hayo yataimarisha ushirikiano wa tamaduni za Kifarsi na Kiarabu na kuimarisha ustaarabu wa Kiislamu.
844357
captcha