IQNA

Mashindano ya Qur'ani kuanza kesho Misri

15:12 - August 17, 2011
Habari ID: 2172732
Sherehe ya kufungua mashindano ya kimataifa ya hifdhi, tajwidi na tafsiri ya Qur'ani Tukufu imepangwa kufanyika mjini Cairo Misri hapo kesho Alkhamisi tarehe 18 Agosti.
Sherehe hiyo itafanyika katika ukumbi wa Muhammad Abduh katika Chuo Kikuu cha al-Azhar. Sherehe ya mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa ushirikiano wa Iswam Sharaf, Waziri Mkuu wa Misri, itahudhuriwa na Ahmad Tayyib, Sheikh wa al-Azhar, Muhammad Abdu al-Fadhil al-Quswei, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Misri pamoja na Waziri mwenzake wa Mambo ya Ndani, viongozi wa ngazi za juu wa Misri pamoja na mabalozi wa nchi za kigeni wanaohudumu Msri na vilevile wahubiri wa kidini wa nchi hiyo.
Mashindano hayo yamepangwa kuendelea hadi tarehe 25 Agosti.
Akibainisha namna mashindano hayo ya 19 yatakavyofanyika, al-Fadhil al-Quswei amesema kuwa wawakilishi 99 kutoka nchi 65 watachuana katika makundi tofauti ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani nzima kwa njia ya tajwidi pamoja na kufasiri juzuu moja, hifdhi inayoandamana na kiraa cha tajwidi ya juzuu 20, na vilevile hifdhi kama hiyo ya juzuu 10 za Qur'ani.
Vilevile kundi maalumu la washiriki wa mashindano hayo kutoka nchi zisizo za Kiarabu limeandaliwa, ambapo washindani watatakiwa kuhifadhi juzuu 6 za Qur'ani Tukufu.
Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Misri amesema kuwa timu ya waamuzi 10 imechaguliwa ili kuendesha mashindano hayo.
Washiriki wa mashindano hayo pia wameandaliwa fursa ya kuyatembelea maeneo ya mambo ya kale nchini Misri. 845034
captcha