IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur'ani Imarati kupongezwa

10:30 - August 19, 2011
Habari ID: 2173062
Washindi wa mashindano ya kimataifa ya Imarati yaliyofanyika chini ya anwani 'Kiraa Bora zaidi cha Qur'ani', ambayo yaliwashirikisha washindani 24 kutoka nchi 9 wanatazamiwa kufanyiwa sherehe maalumu ya kuwapongezatarehe 23 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumzia suala hilo, Ibrahim al-Janabi, mkuu wa kamati ya waamuzi waliosimamia mashindano hayo amesema kuwa mashindano hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya Imarati ya at-Turath, yalikamilika siku ya Jumatatu tarehe 15 Agosti.
Amesema kamati iliyotajwa iliwachagua washindi watatu kutoka makundi mawili, la juu na la mwanzo, kuwa washindi wa mwisho wa mashindano hayo na majina yao yatatangazwa rasmi katika sherehe ya kuwaenzi na kuwatunukia zawadi.
Mshindi wa kwanza atapewa dirham 20,000, wa pili dirham 15000 na wa tatu dirham 10,000 za Imarati. Hao ni washindi wa kundi la juu. Wa kundi la mwanzo watapewa diraham 15,000, 10,000 na dirham 8,000 kwa utaratibu. 845277
captcha