IQNA

Ijumaa ni siku ya kufungamana na watu wa Palestina

13:50 - August 25, 2011
Habari ID: 2176619
Baraza la Maulamaa wa Pakistan, limetangaza kwamba Ijumaa ya kesho ambayo ni ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani itakuwa ni siku ya kufungamana na wananchi wa Palestina wanaokumbwa na machungu makubwa kutokana na jinai zinazotekelezwa dhidi yao na walowezi wa Kizayuni.
Akitangaza suala hilo hivi karibuni mbele ya waandishi habari, mkuu wa baraza hilo ameelezea wasiwasi na masikitiko yake makubwa kuhusiana na unyama na mateso yanayofanywa na wavamizi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
Amesema ratiba ya Siku ya Quds itajumuisha maandamano makubwa katika miji tofauti ya Pakistan na vilevile kuandaa vikao vya hutuba za kuweka wazi jinai, mauaji na mateso wanayofanyiwa Wapalestina na wavamizi wa Kizayuni kwa ushirikiano wa Marekani.
Baraza hilo la Maulamaa wa Pakistan pia limeitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC kuchukua hatua za dharura ili kukabiliana na uchokozi wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi.
Limezitaka nchi zote za Kiislamu na Kiarabu kutoa mashinikizo dhidi ya utawala huo na vilevile kuzuia uungaji mkono na msaada wa hali na mali wa Marekani kwa utawala huo dhidi ya Wapalestina. 849225
captcha