IQNA

Kituo cha mafunzo ya Qur'ani chafunguliwa Chechnia

11:40 - August 28, 2011
Habari ID: 2177915
Kituo cha mafunzo ya Qur'ani Tukufu kilifunguiwa siku ya Ijumaa huko Grozni mji mkuu wa Jamhuri ya Chechnia.
Kituo hicho kimejengwa na kimefunguliwa kwa msaada wa Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Two Circles, kituo hicho ambacho kimepewa jina la Sheikh Zaid bin Sultan kitatumika kwa malengo ya kutoa mafunzo mbalimbali ya Qur'ani.
Rais Ramadhan Qadirov wa Chechnia na Nahyan bin Mubarak Aal Nahyan, Waziri wa Elimu ya Juu na Utafiti wa Kielimu wa Imarati walihudhuria ufunguzi wa kituo hicho.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Rais Qadirov amesema kuwa kituo hicho ambacho kimejengwa kwenye ukubwa wa hekari 40 ndicho kikubwa zaidi cha aina yake katika eneo zima la Caucasia Kaskazini.
Kituo hicho kina majengo mbalimbali yakiwemo ya msikiti, michezo, malazi, madarasa ya mafunzo ya Qur'ani na kadhalika. 850313
captcha