IQNA

Wamisri waanzisha mchakato wa marekebisho ya mkataba wa Camp David

14:58 - September 04, 2011
Habari ID: 2181129
Serikali mpya ya Misri meanzisha mchakato wa marekebisho ya mkataba wa Camp David uliotiwa saini mwaka 1979 kati ya serikali ya wakati huo ya Cairo na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mwanadiplomasia wa ngazi za juu wa Misri Mahmoud Izzat ambaye ni Mkurugenzi wa kitengo cha masuala ya sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo amesema kuwa mkataba wa Camp David utafanyiwa marekebisho kwa mujibu wa masharti yatakayotolewa na serikali ya sasa wa Misri.
Amesema miongoni mwa vipengee vitakavyofanyiwa marekebisho ni pamoja na sheria zinazohusiana na idadi ya askari waliopo katika mpaka wa nchi hiyo na utawala haramu wa Israel kwa ajili ya kudhamini usalama na kadhia ya uuzaji wa gesi ya Misri kwa utawala huo ghasibu.
Mahmoud Izzat amesema kuwa Israel imekiuka mkatabala wa Camp David mara kadhaa kwa kushambulia maene ya mpakani ya Misri na kuua askar jeshi wa nchi hiyo.
Mkataba wa amani wa Camp David ulitiwa saini nchini Marekani mwaka 1979 kati ya kiongozi wa wakati huo wa Misri Anwar Saadat na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Menachim Begin. 854113

captcha