Mkutano huo wa siku mbili umefunguliwa kwa hptuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ambaye amesisitiza kuwa harakati zinazoshuhudiwa hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu zimetokana na mafundisho ya Uislamu na Qur'ani Tukufu.
Mkutano huu unahudhuriwa na wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu na wasio Waislamu kutoka nchi 80 duniani na vilevile wanafikra 400 wa Kiirani.
Katibu Mkuu wa mkutano huo amewaambia waandishi wa habari kwamba, lengo la mkutano huo ni kuandaa mazingira ya kubadilishana mawazo wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu kuhusu mwamko wa Kiislamu. Pia amesema Iran imependekeza kuundwa sekretarieti ya kufuatilia maamuzi yatakayofikiwa katika mkutano huo na kuendelezwa vikao na fikra kama hizo kwa sura tofauti.
861703