Al-Hassanawi amesema, kuna ushahidi na nyaraka za kuaminika zinazoonyesha kwamba al-Qaida nchini Iraq imechukua jukumu la kutekeleza siasa hatari za Marekani nchini Iraq.
Mbunge huyo wa mrengo wa Muqtada Sadr katika Bunge la Iraq amesema kwamba viongozi wa kisiasa na kiusalama wa Iraq wamekuwa wakifuatilia ushahidi na vielelezo vya ugaidi ambavyo vyote vimekuwa vikiishia kwenye kambi za kijeshi za Marekani zilizoko nchini Iraq.
Amesema askari usalama wa Iraq pia wamekuwa wakilalamika kwamba wavamizi wa Marekani nchini humo wamekuwa wakiwapa habari zisizo sahihi kuhusiana na baadhi ya masuala ya kiusalama. Mrengo wa Sadr tayari umetangaza kwamba askari jeshi wa Marekani wana muda wa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu kundoka katika ardhi ya Iraq la sivyo utaamiliana nao kama askari vamizi na kutangaza rasmi vita dhidi yao. 862737