Wachambuzi wa masuala ya kisasa wanasema kuwa Saudia ambayo imekuwa kimbilio la madikteta wa Kiarabu sasa inakariri uvamizi na ukandamizaji inaoufanya dhidi ya wananchi wa Bahrain huko Yemen kwa maslahi ya utawala wa Rais wa nchi hiyo Abdallah Swaleh, ambaye imemfanya kuwa mateka huko Riyadh.
Wanadiplomasia wa kigeni walioko Sanaa wanasema kuwa, askari wa Saudia waliotumwa Yemen wanatumia zana za kisasa kabisa za ukandamizaji ambazo kimsingi zimeagizwa kutoka Ujerumani, Uingereza, Marekani na Ufaransa dhidi ya Wayemen wanaopinga dhulma na udikteta wa Swaleh. Askari hao wamekuwa wakitumia mbinu za kinyama kuua na kumwaga damu ya raia wa kawaida wasio na hatia yoyote isipokuwa kupaza sauti zao dhidi ya dhulma ya dikteta huyo.
Maujai ya zaidi ya Wayemen 50 katika kipindi cha chini ya siku moja yametekelezwa na Wasaudia kutokana na ukweli kuwa askari wa Yemen wamekataa kuwafyatulia risasi ndugu zao. 864197