IQNA

Iraq yawapa magaidi miezi mitatu kuondoka nchini humo

13:58 - September 22, 2011
Habari ID: 2191876
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq imewapa magaidi waliokimbia Iran wanaojiita Mujahidina Khalq wanaoishi nchini humo kwa msaada na uungaji mkono wa nchi za Magharibi na hasa Marekani, muda wa miezi mitatu wawe wameondoka katika ardhi ya nchi hiyo.
Akisoma taarifa ambayo inabainisha msimamo wa hivi karibuni wa serikali ya Iraq kuhusiana na magaidi hao ambao wametoa roho za viongozi na raia wengi wasio na hatia wa Iran, Lubeid Abawi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq amesisitiza kwamba magaidi hao wamepewa fursa ya hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wawe wameondoka katika ardhi ya nchi hiyo. Amesema kuwa serikali ya Baghdad imechukua uamuzi wa kufunga kambi ya magaidi hao ya Ashraf kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Abawi amesema kundi hilo linatambuliwa kuwa la kigaidi na hata waungaji mkono wao wakuu wa Magharibi na kwa hivyo hawapasi kuwa katika ardhi ya Iraq kwa sababu wamemwaga damu ya watu wengi wasio na hatia na kushirikiana na utawala wa dikteta Saddam Hussein katika kutekeleza jinai nyingi dhidi ya Waislamu.
Hata hivyo amesema kwamba serikali ya Iraq iko tayari kushirikiana na shirika linalohudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR katika kuamiliana kibinadamu na kundi hilo kwa kulipa makazi kwingineko. 865512
captcha