Rais Ahmadinejad ambaye yuko New York, Marekani kushiriki katika kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema katika mahojiano aliyofanyiwa na vyombo vya habari vya kimataifa kwamba, kama Marekani, Uingereza na NATO zitaondoka katika Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman, Iran ikishirikiana na nchi za eneo hilo zinaweza kudhamini usalama wa nishati ya eneo.
Rais Ahmadinejad amesema, baadhi ya madola ya kigeni yako katika eneo la Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman kwa kisingizio cha kudhamini usalama wa nishati na ya eneo hilo; lakini ameitaka NATO na Marekani kuondoka katika eneo hilo na kwamba, masuala hayo yanaweza kudhaminiwa na nchi husika.
Rais Ahmadinejad amesisitiza pia kuunga mkono mamlaka ya kujitawala Palestina, haki ya kila nchi kunufaika na urutubishaji madini ya Urani na akasema makelele ya madola ya kibeberu kuhusiana na miradi ya nyuklia ya Iran hayana maana; kwani shughuli za nyuklia za taifa hili zinafanyika chini ya usimamizi kamili wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki.
866525