Huku akisisitiza kwamba umoja na mapatano ya kitaifa ni mambo mawili yenye umuhimu mkubwa kwa ajili ya kupatikana ushindi wa Wapalestina dhidi ya utawala haramu wa Israel, Ahmad Tayyib amewataka viongozi wote wa Palestina kuungana na kufikia mapatano ya umoja wa kitaifa haraka iwezekanavyo.
Amesema Al-Azhar inaunga mkono juhudi zote za kuvunja mzingiro unaotekelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukada wa Gaza na kusema kuwa tasisi hiyo ya kidini hata inashirikiana na misafara ya misaada ya kimataifa inayoelekea huko kwa sababu hilo ni jambo la fahari kwa taasisi hiyo.
Sheikh wa al-Azhar siku ya Jumatatu alikutana na kuzungumza na Ekeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikaino wa Kiislamu ambapo alilaani shambulio lilofanywa hivi karibuni na Mayahudi wenye misimamo ya kupindukia dhidi ya maeneo ya ibada ya Waislamu huko Palestina.
Viongozi wawili hao walijadili masuala tofauti yanayouhusu ulimwengu wa Kiislamu yakiwemo ya kuondoa picha mbovu iliyoko katika jamii za Magharibi kuhusiana na Uislamu, kutekelezwa mipango ya pamoja kwa lengo la kulinda matukufu na thamani za Kiislamu na hasa suala la Quds Tukufu na kuzisadia nchi za Kiislamu kukabiliana na njaa pamoja na majanga tofauti ya kimaumbile. 873988