Vijana hao wametaka kuhukumiwa kisheria kwa nchi zote za Magharibi zinazotoa fedha na silaha kwa makundi ya kigaidi ili yavuruge usalama na uthabiti wa nchi hiyo.
Akizungumza katika mkusanyiko huo wa malalamiko Ahmad al-Ahmad, Katibu Mkuu wa Harakati ya Wasoshalisti wa Kiarabu, amesema kuwa Syria itaendelea kupeperusha bendera ya utukufu wa umma wa Kiarabu. Amesema kuwa vijana wa Syria wanazikosoa vikali taarifa zinazotolewa na duru zinazojiita kuwa jamii ya kimataifa kwa sababu zinafungamana moja kwa moja na Marekani.
Vijana hao wamezikosoa nchi za Magharibi na Kiarabu kwa kushirikiana katika kuendesha wimbi kubwa la propaganda dhidi ya Syria kwa lengo la kuilazimisha isalimu amri na kuacha kuunga mkono mapambano ya Kiislamu dhidi ya utawala haramu wa Israel.
Mamilioni ya wananchi wa Syria hapo jana Jumatano pia walifanya maandamano makubwa ya kuonyesha uungaji mkono wao kwa serikali ya Rais Bashar al-Asad. 878858