IQNA

Mamilioni ya dola ya watoto wa Mubarak yakatwa katika benki za Uswisi

21:59 - October 18, 2011
Habari ID: 2207552
Maafisa wa Misri wameripoti kuwa wana wa kiume wa Hosni Mubarak dikteta aliyeng'olewa madarakani nchini humo wana mamilioni ya dola katika akaunti za benki mbalimbali za Uswisi.
Assemm al Gohari Naibu Waziri wa Sheria wa Misri amesema kuwa Gamal Mubarak na mdogo wake Alaa wana kiasi cha dola milioni 340 katika benki za Uswisi. Amesema kamati ya kudhibiti mapato ya Misri imepokea taarifa zinazothibitisha kuwa watoto hao wa kiume wa Mubarak wana akiba ya dola milioni 340 katika benki ya Uswisi, ambapo dola milioni 300 zimetajwa kuwa mali ya Alaa.
Naibu Waziri wa Sheria wa Misri ambaye pia ni mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Mapato Haramu ya nchi hiyo ameongeza kuwa Alaa ambaye yuko mbaroni nchini Misri pamoja kaka na baba yake kwa tuhuma za ubadhirifu na utumiaji mbaya wa madaraka, atakabiliwa na tuhuma za usafishaji wa pesa nchini Uswisi. Ameongeza kuwa serikali ya Uswisi ilizuia mali zenye thamani ya dola milioni 450 mali ya familia ya Hosni Mubarak na viongozi wengine wa utawala wa zamani wa Misri, baada dikteta huyo kung'olewa madarakani mwezi Februari mwaka huu.882531


captcha