Akibainisha suala hilo Jamil Haik amesema kuwa kuanguka na kuangamia kwa madikteta wote ni jambo lisilo na shaka na kuwa kifo cha Gaddafi ni mwanzo wa kukombolewa Imam Musa Sadr na wenzake. Amesema Walebanon watafanya kila wawezalo ili kuhakikisha kuwa mwanazuoni huyo na mateka wenzake wanarudi nyumbani wakiwa salama salmini.
Katika sehemu nyingine ya matamshi yake, Haik amesema kwamba mataifa ya Kiislamu ya Mashariki ya Kati yanafanya juhudi kubwa za kuvunja njama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi yao. Amesema tawala na taasisi za Kiarabu za eneo la Mashariki ya Kati zinapasa kurejesha imani ya wananchi kwao na kujiepusha kutumiwa vibaya na madola makubwa ya Magharibi.
Ameashiria pia machafuko ya hivi karibuni kati ya polisi na Makopti wa Misri na kusema kwamba machafuko hayo yalichochewa na Wazayuni wa Israel ili kuchafua jina la mapinduzi ya wananchi wa Kiislamu wa nchi hiyo, wananchi ambao hivi karibuni waliteremsha na kuchoma bendera ya utawala huo haramu mjini Cairo. 885050