Waislamu wa Marekani wamejiunga na Wamarekani wenzao katika kulalamikia dhulma na ukosefu wa usawa wa kiuchumi wa mfumo wa kibepari katika harakati iliyopea jina la kuteka nyara Wall Street, makao makuu ya shughuli za kiuchumi na kifedha huko Marekani.
Linda Sarsor Mkuu wa Jumuiya ya Waarabu wa Marekani amesema kuwa Waislamu wa New York wanakusanyika leo kutangaza muungano wao na harakati ya kuteka nyara Wall Street.
Wanachama wa Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani (CAIR) na Baraza la Uongozi wa Kiislamu la New York pia wametangaza uunganji mkono wao kwa maandamano na malalamiko ya wananchi wanaopinga mfumo wa kibepari wa Marekani.
Maelfu ya wananchi wa Marekani katika wiki za hivi karibuni wamekuwa wakifanya maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hiyo wakilalamikia dulma na ukosefu wa uuadilifu wa mfumo wa kibepari unaotawala nchi hiyo, umaskini na vifo vinavyosababishwa na hali hiyo. 886154