IQNA

Australia mwenyeji wa kongamano la kimataifa la Uislamu na Ulaya

11:28 - October 30, 2011
Habari ID: 2214186
Kongamano la kimataifa la 'Uislamu na Ulaya: Utamaduni, Historia na Siasa' limepangwa kufanyika nchini Australia tarehe 8 na 9 za mwezi Machi mwakani.
Kwa mujibu wa tovuti ya EuroIslam, kongamano hilo limeandaliwa na Kundi la Utafiti la Ulaya kwa ushirikiano wa Kundi la Utafiti wa Kiislamu na Kiarabu la Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Australia kwa lengo la kuchunguza hali ya Waislamu barani Ulaya na uhusiano wa bara hilo na ulimwengu wa Kiislamu.
Madhebu na tamaduni tofauti katika Uislamu, Waislamu, jamii ya kiraia, demokrasia na usekula, athari ya Uislamu kwa historia ya Ulaya, matukio ya hivi karibuni ya Mashariki ya Kati na utambulisho wa kiutamaduni na sanaa ni miongoni mwa masuala muhimu yatakayojadiliwa katika kongamano hilo la siku mbili.
Wahadhiri wa masuala ya utafiti wa Kiislamu, Mashariki ya Kati na Ulaya na vilevile wataalamu wa masuala ya kijamii kutoka vyuo vikuu tofauti vya dunia watashiriki katika kongamano hilo la kimataifa. 888965
captcha