Kongamano hilo ambalo limehudhuriwa na zaidi ya Waislamu elfu mbili limefanyika kwa shabaha ya kupambana na ubaguzi unaofanywa dhidi ya Waislamu na kuwazindua watu kuhusu hatari ya kuwepo masuala kama hayo katika jamii ya Uswisi.
Niclas Blanchor Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Uswisi alihutubia kongamano hilo akisema kuwa Waislamu wa nchi hiyo wanaitambua marufuku ya ujenzi wa minara ya misikiti kuwa ni ubaguzi unaofanywa dhidi yao na sehemu moja ya propaganda za kutaka kuwatisha watu kuhusu Uislamu.
Amesema, Waislamu wa Uswisi hawapasi kutambuliwa kama raia wa daraja la pili. Amesema kuwa raia Waislamu wanabaguliwa katika mazingira ya kazi, duru za kijamii, michezoni na hata katika ofisi za serikali na sasa wakati umefika wa kuchukuliwa hatua za kupambana na ubaguzi huo.
Lauren Booth dada wa mke wa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ambaye alisilimu na kukubali dini ya Kiislamu baada ya kutembelea mji mtakatifu wa Qum alikuwa miongoni mwa wageni wa kongamano hilo.
Viongozi wa dini za Kikristo na Kiyahudi pia walihutubia kongamano hilo wakisisitiza juu ya udharura wa kupambana na propraganda chafu zinazofanywa dhidi ya Waislamu na dini yao, ubaguzi na vitendo vya kutumia mabavu. 889552