IQNA

Warsha ya mafunzo ya kuhifadhi turathi za Kiislamu yafanyika Ghana

15:31 - October 31, 2011
Habari ID: 2215199
Warsha ya mafunzo ya kuhifadhi turathi za Kiislamu ilifanyika hivi karibuni katika mji wa Kumasi nchini Ghana.
Warsha hiyo iliandaliwa kwa madhumuni ya kuwasilisha njia bora za kulinda turathi na athari za Kiislamu.
Warsha hiyo ambayo imedhaminiwa na Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani imewasilisha njia za kulinda na kuhifadhi maandishi ya mkono, nuskha za chapa, ramani na vitabu adimu vya Kiarabu na Kiislamu.
Warsha hiyo imefanyika wa ushirikiano wa ofisi ya mufti mkuu wa Ghana. Wasimamizi wa warsha hiyo wamesema kuwa wamelazimika kuandaa warsha hiyo kutokana na kuharibika turathi nyingi za Kiislamu nchini, jambo ambalo limesababishwa na kutokuwepo ujuzi wa kutosha wa kuhifadhi maandishi na turathi za kale za Kiislamu.
Watu walioshiriki kwenye warasha hiyo watasaidia katika kuwafunza wenzao namna ya kulinda turathi za Kiislamu. 890032
captcha