Akizungumza mbele ya waandishi habari katika mji wa Tripoli, Jibril amesema kuwa kila kamati ya kigeni inayojishughulisha na masuala tofauti nchini Libya itapasa kutekeleza majukumu yake chini ya usimamizi wa Baraza la Mpito ili kulinda maslahi ya kitaifa ya nchi hiyo.
Amesema baraza hilo linatilia maanani masuala muhimu ya nchi hiyo likiwemo faili la Imam Musa Sadr na kuongeza kuwa suala hilo linashughulikiwa na kamati maalumu ambayo imebuniwa na baraza hilo la mpito.
Amesema kufikia sasa amezungumza mara mbili kwa njia ya simu na Najib Miqati, Waziri Mkuu wa Lebanon na kumfahamisha juhudi ambazo zinafanyika kwa ajili ya kushughulikia faili hilo muhimu. Ameongeza kuwa kutafutiwa ufumbuzi suala hilo kutakuwa na maslahi kwa nchi zote mbili.
Jibril amesema suala hilo linapasa kutatuliwa haraka iwezekanavyo ili kuondoa vizuizi vinavyozuia kuimarishwa uhusiano wa nchi mbili hizo muhimu za Kiarabu. 890386