IQNA

Indonesia yatangaza Jumapili ijayo kuwa Idi

16:12 - November 01, 2011
Habari ID: 2215777
Makundi muhimu ya Kiislamu ya Indonesia yametangaza kuwa yameafikiana kutangaza siku ya Jumapili ijayo tarehe 6 Novemba kuwa siku ya kusherehekea sikukuu ya Idul Adh'ha.
Kwa mujibu wa gazeti la Jakarta Globe, Makundi mawili ya Kiislamu ya an-Nahdhat al-Ulamaa na Muhammadiya ambayo yalihitilafiana kuhusiana na siku ya kusherehekewa Idul Fitr ya mwaka huu, yamekubaliana kusherehekea siku ya Jumapili ijayo kama siku ya Idul Adh'ha.
Sha'la Hayat mmoja wa wanachama wa kundi la an-Nahdhat al-Ulamaa katika eneo la Java Mashariki amesema kuwa uchunguzi wa nujumu na mahesabu yanabaini kwamba siku ya Jumapili ijayo ndiyo itakayokuwa siku ya Idul Adh'ha.
Mwaka huu zaidi ya Waindonesia laki mbili, ambayo ni nchi iliyo na Waislamu wengi zaidi duniani, wanashiriki katika hija ya mwaka huu. 891066
captcha