Nayif bin Abdul Aziz ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudia amesema kuwa nchi hiyo haitaruhusu harakati ya mabadiliko iliyozikumba nchi kadhaa kuhamia nchini humo kupitia kwa mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu.
Nayif bin Abdul Azizi amewataka mahujaji kusahau kabisa mwamko wa Kiislamu na mageuzi ya kimapinduzi katika siku za ibada ya Hija.
Amesisitiza kuwa serikali ya Saudi Arabia imejitayarisha kukabiliana na malalamiko ya aina yoyote wakati wa ibada ya Hija.
Vyombo vya habari vya Saudia vinasema askari laki moja na nusu wametayarishwa kwa ajili ya kusimamia usalama wakati wa ibada ya hiyo. 891951